Tuesday, 14 June 2016
Halotel kufikisha mtandao kwa asilimia 95 ya watanzania hadi mwishoni mwa mwaka 2016
Naibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akizungumza
na wanahabari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
leo kuhusuiana na mtandao huo kutanua huduama zake hadi kufikia asimimia
95 ya watazanzania. Wanaoshuhudia ni Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali
Watu, Emanuel Malyeta (kushoto), na kulia kwake ni mwanasheria wa
kampuni hiyo,Christopher Masai.
Naibu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Halotel, Emanuel Malyeta akifafanunua
jambo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni
ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai kulia kwake ni mwanasheria wa
kampuni hiyo,Christopher Masai.
Naibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akimkabidhi
zawadi mwandishi wa gazeti la the Guardian, Sylivester Domaso.
Dar es Salaam, 5/1/2016: Kampuni
mpya ya simu za mikononi, Halotel, leo imetangaza mpango wake wa
kufikisha mtandao wa simu kwa asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu. Wakiongozwa na kauli mbiu yao ya Pamoja katika Ubora, wanalenga
kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata
huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa
imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo
havikuwa vimeunganishwa na huduma ya mtandao awali.
Hadi
sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka
sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano,
kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa
yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95%
ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.
Akizungumzia
mipango ya kampuni yake kwa mwaka 2016, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu
wa Halotel, bwana Le Van Dai amesema kampuni yake itaendelea kupeleka
mtandao katika vijiji vingine 1500 katika mwaka 2016 na kuweka mkazo wa
hali ya juu katika mrejesho kwa wateja pamoja na kuboresha mtandao,
huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika
sekta ya mawasiliano nchini.
‘Kampuni
yetu itashirikiana na watanzania katika kuhakikisha inaleta maendeleo
kwa watanzania, kama ambavyo kauli mbiu yetu ilivyo, Pamoja katika
Ubora, ndivyo ambavyo tutaendelea kuwekeza hapa nchini hali
itakayopelekea kukua haraka kwa kampuni yetu’ alisema Bwana Dai.
Katika
hatua nyingine Dai amewashukuru watanzania na serikali yao kwa mapokezi
waliyoipa kampuni yao, na pia amewahakikishia kuwa Halotel itaendelea
kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na wataendelea kushirikiana
nao katika kusukuma maendeleo ya nchi.
‘Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano
mkubwa waliotupa, na kuelekea mwaka 2016, kampuni yetu itaendelea kukuza
ubunifu, zawadi pamoja na huduma nyingine kwa wateja wetu’ alisema Dai.
Kwa
mwaka 2015 pekee, kampuni ya Halotel imelipa kodi ya zaidi ya dola
milioni 27 za kimarekani, ambayo kati ya hiyo dola milioni 24 imetumika
kulipa kodi uingizaji bidhaa na dola laki saba ni kodi inayohusuiana na
rasrimali watu.
Dai
amesema pia kampuni yake imetengeneza zaidi ya ajira 1,500 za moja kwa
moja na zaidi ya 20,000 za ajira zisizo za moja kwa moja, akisisitiza
kuwa kampuni yake itahakikisha inafata sheria za ajira za Tanzania.
Katika
hatua nyingine, Dai alielezea masikitiko yake kwa matukio ya wizi na
uporaji wa mitambo ya Halotel, akielezea kuwa zaidi ya matukio 52
yameripotiwa kuanzia mwezi wa kwanza hadi Disemba mwaka huu, ambapo
imewasababishia hasara ya jumla ya shilingi milioni 393.Lengo la
Halotel ni kuhakikisha kila mtanzania ana simu ya mkononi ili
kubadilisha namna watanzania wanaishi na namna wanavyokuza na kujenga
uchumi wao.
‘Kampuni
yetu ina zaidi ya kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya
minara 2500, hivyo kuifanya Halotel kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa
zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150,
hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya
bure kwa shule zaidi ya 450’ alimaliza Dai.
CCTV & IT TECHNOLOGY
WE ARE DEALING WITH:
1.CCTV CAMERA installation and repair.{CAMERA ZA ULINZI}
2.Cabling installation and Network configuration {CREATING LAN}
3.Landline installation and configuration {SIMU ZA MAOFISINI}
4.Computer Service
-Repair
-Troubleshooting
-Maintenance
Tukifunga CCTV CAMERA ndani ya miezi sita{6} zitakuwa chini yetu endapo itatokea tatizo.
CONTACT:
MOBILE -+255(0) 657 861 947
-+255(0) 625 907 067
EMAIL -cctvittechnology@yahoo.com
TUNAJARI WATEJA, LINDA MALI ZAKO KISASA NA CCTV CAMERA.
WE ARE DEALING WITH:
1.CCTV CAMERA installation and repair.{CAMERA ZA ULINZI}
2.Cabling installation and Network configuration {CREATING LAN}
3.Landline installation and configuration {SIMU ZA MAOFISINI}
4.Computer Service
-Repair
-Troubleshooting
-Maintenance
Tukifunga CCTV CAMERA ndani ya miezi sita{6} zitakuwa chini yetu endapo itatokea tatizo.
CONTACT:
MOBILE -+255(0) 657 861 947
-+255(0) 625 907 067
EMAIL -cctvittechnology@yahoo.com
JIJI LA MWANZA LAFIKIWA NA HUDUMA ZA INTANETI YA KASI YA TIGO 4G LTE
Waandisi wa habari wakifuatilia mkutano huo |
Subscribe to:
Posts (Atom)